Jamaa jina lake anaitwa Ipupa Nsimba aka fally ipupa aka “DiCaprio” aka “La Merveille” alizaliwa pale Kinshasa mnamo Desemba 14 1977.Ni mwimbaji na ni mpiga Guitar mwenye kipaji cha hali ya juu sana.
Alikuwa ni mmoja wa wasanii wa kundi la Quartier Latin kwa takribani miaka 10 alikuwa akifanya kazi zake na Koffi Olomide.Ametengeneza nyimbo kadhaa zilizo hit akiwa na Koffi moja wapo ni Eternellement on Force de Frappe ya mwaka 2001 et Ko Ko Ko Ko on Affaire d’Etat.Aliachia album yake ya kwanza iliyoitwa Droit Chemin ambayo iliuza zaidi ya copies 100,000.
Jamaa amefanya ngoma moja kali zana na Olivia wa G Unit inayoitwa Arsenal de Belles Mélodies ngoma imekamata si kitoto,pia unaweza kumcheki hapa http://www.fally.cd
Facebook Fally Ipupa’s Official Page

No comments:

Post a Comment

WANAUME FAMILY B4 HAWAJA SEPARATE

WANAUME FAMILY B4 HAWAJA SEPARATE
Jamaa walikuwa poa sana lakini mwisho wao nao ulifika basi kila mmoja akijichenga kivyake ila jamaa walitaka kujaribu mziki wa Majita TMK

NDIO ZETU KUWAKIMBIZA

My photo
DAR ES SALAAM, TEMEKE, Tanzania
KUNDI LA TMK MAJITA ORIGINAL,LILIANZISHWA MIAKA SABA ILIYOPITA PALE MAENEO YA KEKO FLATS,KUNDI LILIANZA NA WASANII KUMI,LAKINI TULIFANYA MCHUJO MPAKA WAKABAKIA WASANII SITA.MPAKA SASA TUNA ALBUM MOJA INGAWA HAIJAINGIA SOKONI LAKINI BAADHI YA NYIMBO ZIMESHATOKA RADIONI.WAJUE WASANII WA TMK MAJITA ORG:-ENO K,FRED FID,SOULDIER,KINDAGO,JOSE A.K.A KAMOJA NA DIBWIZZLE

SAUTI ZA BUSATA YARUDI TENA

SAUTI ZA BUSATA YARUDI TENA
ULE WAKATI WA KUPATA KITU ROHO INAPENDA UMESHAWADIA TENA.LILE TAMASHA KUBWA LINALO FANYIKA KILA MWAKA KULE ZANZIBAR LINAKUJIA TENA MWAKANI MWEZI WA 2,TAFADHALI USIKOSE

MDAU ENO K

MDAU ENO K
Jamaa ndie kiongozi wa kundi zima la Majita Original

BASHAM

BASHAM
Washkaji wanaiwakilisha vizuri sana Keko Machungwa.Hip Hop ipo damuni sidhani kama tunaweza kuiacha,hayo ni maneno ya mmoja wao wakati akiongea na mdaku

2 PAC & B.I.G

2 PAC & B.I.G
Hivi hawa jamaa wangekuwepo mpaka leo ingekuwaje?pliz ebu tunaomba maoni yako

EAST COAST TEAM (ECT)

EAST COAST TEAM (ECT)
Jamaa walichengua sana katika anga la mziki wa kibongo lakini mmmhhhh sijui shetani alitoka wapi tena mna aliwamega wao walio imba ama zangu ama zao ila ni mzuka sana kama watakuwa tena pamoja

TMK MAJITA KUPAGAWISHA CHANIKA

TMK MAJITA KUPAGAWISHA CHANIKA
Kundi zima la TMK MAJITA ORIGINAL linategemea kufanya show ya kufa mtu katika kusherehekea sikukuu ya X Mass kule chanika katika ukumbi wa BUTIAMA VILLA siku ya Ijumaa tarehe 25/12/2009 kiingilio ni sawa na bure,wakubwa ni buku 3000 tu na kutakuwa na disco toto kwa kiingilio cha Tsh 1000 tu wasanii kibao kutoka pande hizo watapamba jukwaa,nyote mnakaribishwa